Top 10 similar words or synonyms for umakinifu

kiutendaji    0.857335

unafaa    0.849999

tuwe    0.848120

isiyoweza    0.846126

kushughulikiwa    0.838773

kimawazo    0.826125

linatakiwa    0.825778

kumuelekeza    0.821611

uangalifu    0.819234

kutiliwa    0.817926

Top 30 analogous words or synonyms for umakinifu

Article Example
Tatizo la Kupepesuka lenye Ukosefu wa Umakinifu Kupepesuka kunaweza kuwa na manufaa tukiangazia mtazamo wa kinadharia, katika hali zinazohusisha hatari, mashindano au tabia isiyoeleweka (yaani kutafuta maeneo mapya au kutafuta asili mpya ya vyakula). Katika hali hizi, TKUU inaweza kuwa na manufaa katika jamii huku ikiwa hatari kwa mtu binafsi. Isitoshe, katika mazingira mengine, hali hii inaweza kumnufaisha mtu binafsi, kwa mfano mwitiko wa haraka kwa hatari au stadi kuu ya uwindaji.
Tatizo la Kupepesuka lenye Ukosefu wa Umakinifu Watoto wachache wanaweza kuonyesha kuathiriwa na rangi za chakula na dawa za kuhifadhi. Kuna uwezekano kuwa baadhi ya rangi za chakula zinaweza kuwa kichocheo kwa watu wenye hatari ya kijenetiki. Uiengereza na Shirika la Uropa imeweka hatua za urekebishaji kutokana na madai haya. Sukari inayopendekezwa ya lishe, na kikoleza utamu cha aspartame huonekena kuwa na kiwango kidogo cha athari au kukosa athari; isipokuwa katika watoto wa chini ya miaka sita, ambapo huenda sukari ikaongeza kiwango cha kutomakinika.
Tatizo la Kupepesuka lenye Ukosefu wa Umakinifu Pathofisiolojia ya TKUU si wazi kwani kuna maelezo mengi yanayobishana. Katika watoto wenye TKUU, kuna upungufu wa kijumla wa kiwango cha ubongo, pamoja na ongezeko sawa katika upungufu wa kiwango cha upande wa kushoto wa koteksi inayoitangulia sehemu ya mbele. Njia za ubongo zinazounganisha koteksi iliyoitangulia sehemu ya mbele na striatamu pia hukisiwa kuhusika. Hii inadokeza kuwa kukosa umakinifu, kupepesuka na usukumizi unaweza kuashiria kuathirika kwa ndewe ya mbele, huku sehemu za ubongo kama vile serebelamu pia ikiathirika. Mifumo ingine ya ubongo inayohusishwa na umakinifu pia imetambulika kuwa tofauti katika watu wenye TKUU na wasio nayo.
Tatizo la Kupepesuka lenye Ukosefu wa Umakinifu Dalili za TKUU kama vile kiwango cha chini cha hisia na mtazamo duni wa mtu binafsi, mabadiliko ya hisia na kukasirika zinaweza kukanganywa na disthimia, siklothimia au tatizo la hisia mseto pamoja na tatizo la nafsi la hisia dhaifu. Baadhi ya dalili zinazotokana na matatizo wa kihisia, tatizo la kutohusiana na watu, ulemavu wa ukuaji au ulemavu wa akili au athari za matumizi ya dawa za kulevya kama vile ulevi na kujitenga zinaweza kuingiliana na baadhi ya zile za TKUU. Matatizo haya wakati mwingine yanaweza kutokea pamoja na TKUU. Hali za kimatibabu zinazoweza kusababisha dalili za aina ya TKUU zinajumuisha: uthiroidi, matatizo ya tukutiko, kiwango cha kusumisha cha ledi, upungufu wa uwezo wa kusikia, ugonjwa wa ini, apnea ya usingizi, miingiliano ya dawa, na jeraha la kichwa.
Tatizo la Kupepesuka lenye Ukosefu wa Umakinifu Ufuatiliaji wa miaka minane katika watoto waliotambuliwa kuwa na TKUU (aina changamani) uligundua kuwa watoto hawa huwa na matatizo mara nyingi katika ujana iwapo watapata matibabu au la. Barani Marekani, chini ya asilimia 5 ya watu wenye TKUU hupata shahada ya chuo kikuu, ikilinganishwa na asilimia 28 ya idadi jumla wenye umri wa miaka 25 na zaidi. Idadi ya watoto wanaofikia kigezo cha TKUU hushuka hadi nusu katika miaka mitatu kufuatia utambuzi. Hali hii hutokea pasi kutegemea matibabu yanayotumika. TKUU huendelea kuwepo katika utu uzima katika takriban asilimia 30 hadi 50 ya visa. Waathiriwa wana uwezekano wa kukuza mbinu za kuhimili wanapokomaa, hivyo kufidia dalili zao za awali.
Tatizo la Kupepesuka lenye Ukosefu wa Umakinifu Mara nyingi kutomakinika, kupepesuka (kutotulia kwa watu wazima), tabia ya kuzua vurugu na usukumizi wa ghafla hupatikana katika TKUU. Kutatizika katika masomo hutokea mara nyingi sawia na matatizo ya kimahusiano. Dalili zinaweza kuwa ngumu kufasili kwa sababu ya ugumu wa kutambua mwanzo wa viwango vya kawaida vya kutomakinika, kupepesuka na mwisho wa usukumizi na viwango muhimu vinavyohitaji usaidizi. Ili hali hii kutambulika, ni sharti dalili hizi zidhihirike katika mandhari mawili tofauti kwa miezi sita au zaidi na katika kiwango kilicho juu ya kile cha watoto wengine wa umri sawa.TKUU linaweza kuainishwa katika aina tatu kulingana na dalili zinazojidhihirisha—linalozidisha kutomakinika, la kupepesuka na usukumizi, au aina changamani ikiwa vigezo vya aina zote mbili zifikiwa.
Tatizo la Kupepesuka lenye Ukosefu wa Umakinifu Uzito wa chini sana wa wakati wa kuzaliwa, kuzaliwa kabla ya wakati na shida za mapema pia huongeza hatari sawia na maambukizi katika ujauzito, wakati wa kuzaa na katika utotoni. Baadhi ya maambukizi haya yanajumuisha: virusi mbalimbali (ukambi, tetekuwanga, rubela, enterovirusi 71) na maambukizi ya bakteria ya streptokokali. Angalau asilimia 30 ya watoto wenye majeraha ya ubongo hupata TKUU baadaye na takriban asilimia 5 ya visa husababishwa na majeraha ya ubongo.
Tatizo la Kupepesuka lenye Ukosefu wa Umakinifu Kulingana na nadharia ya muundo wa jamii, jamii huamua mipaka kati ya tabia ya kawaida na isiyo ya kawaida. Watu katika jamii: ikijumuisha matabibu, wazazi na walimu huamua vigezo vitakavyotumika, na hivyo, idadi ya watu walioambukizwa. Matokeo ya hali hii ni kigezo cha DSM IV hufikia viwango vya TKUU mara tatu hadi nne zaidi kuliko cha ICD 10. Thomas Szasz, muunga mkono wa nadharia hii, amesema kuwa TKUU "ilibuniwa na wala si kutambuliwa."
Tatizo la Kupepesuka lenye Ukosefu wa Umakinifu Inapendekezwa kuwa hali zinazohusishwa zichunguzwe, kama vile: hisia, mfadhaiko, tatizo la ukaidi wa kiupinzani na tatizo la mwenendo, aidha matatizo ya kujifunza na ya lugha. Matatizo zaidi yanayopaswa kuchunguzwa yanajumuisha: matatizo mengine ya ukuaji wa nyuro, mtetemo wa kineva, na apnea ya usingizi.
Tatizo la Kupepesuka lenye Ukosefu wa Umakinifu Matatizo ya usingizi ya kimsingi yanaweza kuthuru umakinifu na mtindo na dalili za TKUU zinaweza kuathiri usingizi. Hivyo, inapendekezwa kuwa watoto wenye TKUU wakadiriwe kila mara kuhusu matatizo ya usingizi. Usingizi mwingi katika watoto unaweza kusababisha dalili za kimsingi kama vile kupiga miayo na kusugua macho, usukumizi, kupepesuka, uchokozi, mabadiliko ya hisia na kutomakinika. Apnea tata ya usingizi pia inaweza kusababisha dalili za aina ya TKUU.