Top 10 similar words or synonyms for sax

palla    0.957522

suzy    0.956601

creature    0.953477

tumbe    0.953000

chaurembo    0.952718

zonga    0.951210

haroub    0.951150

ameir    0.950989

kimaro    0.950222

zaynab    0.949429

Top 30 analogous words or synonyms for sax

Article Example
Mafumu Bilali Mafumu Bilal Bombenga al-maarufu Super Sax ni mwanamuziki maarufu wa muziki wa dansi kutoka jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Kanku Kelly Mwaka 1982 Kanku alichumpa hadi Nairobi nchini Kenya, na akajiunga na bendi ya Orchestra Virunga iliyokuwa ikiongozwa na mwanamuziki mkongwe Samba Mapangala, ambako alidumu na bendi hiyo kwa takriban miaka miwili. Akiwa huko Kenya mwaka 1984 Nkashama Kanku Kelly akiwa na wanamuziki wenzake, waliamua kuanzisha bendi yao ya Orchestra Vundumuna ikiwa na wanamuziki nguli akina Sammy Kasule (kuimba), Nsilu wa Bansilu ‘Manicho’(gita), Tabu Ngongo(sax), na Tabu Fratal (gita/drums). Wengine walikuwa akina Munamba Jean (keyboard) na Botanga Mofrank Bijing, ambaye alikuwa kiongozi wa bendi na mpiga keyboard. Anamtaja Mofank kuwa ndiye aliyekuwa chanzo cha bendi hiyo kupata mikataba wa kupiga muziki nchini Japan kwa kupitia nafasi yake ya kuoa mwanamke wa nchi hiyo.
Washirika Tanzania Stars Mambo yakaenda yakiongezeka! Lakini si kwa mema. Kizaazaa kwenye bendi hiyo kikatokea mwaka 1993 wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, ambao mara nyingi huwa ni likizo kwa wasanii wote kutokana na watu wengi kufunga, hususan waumini wa Kiislamu, hivyo burudani zote hupungua. Wanamuziki wa bendi hiyo walipoanza kudai ‘mafao’ yao ili waende likizo, viongozi wa Ushirika wakaweka ngumu na kutaka waendelee kutumbuiza! Wanamuziki walijitahidi kuuelewesha uongozi kwamba kipindi hicho mapato huwa haba kutokana na wapenzi wengi wa dansi kuwa katika funga ya Ramadhan. Lakini viongozi hao hawakusikia la Muadhini wala Mnadi Swala! Wakwaambia wanamuziki, kwamba mlango uko wazi, anayetaka kuondoka aondoke, anayetaka kubaki, apige kazi kama kawaida. Waliobaki wakabaki, walioondoka wakaondoka. Mwaka wa 1994, Adam Bakari, mwanamuziki huyo alisema kwamba aliamua kumwendea rafiki yake aitwaye Mwakibinga na kumshawishi waanzishe bendi, naye bila hiyana akaridhia na kutafuta vyombo Sinza kwa Mzee Mbaga, ambavyo walivinunua kwa Shs. 2 milioni tu. Kama masikhara vile, wakaanzisha bendi ya MCA International mwaka 1994, ambayo iliundwa na yeye Sauti ya Zege, Said Makelele (tarumbeta), Abdallah Kimeza (sax), Noordin Athumani (rhythm), George Kessy Omojo (bass), na Kassim Rashid Kizunga (solo), ambaye alikuwa amechukua nafasi ya Kalala kule Washirika katika awamu ya pili. Bendi ya MCA International ikaweka kambi yake Bagamoyo. Washirika Tanzania Stars ikabaki ikisuasua tu pamoja na jukumu la kuiendeleza kukabidhiwa Zahir Ally Zorro na Hassan Show. Zorro akaibuka na kibao cha ‘Mikufu ya Dhahabu’, lakini juhudi zake hazikuzaa matunda na hatimaye bendi hiyo ikatoweka kwenye anga la muziki wa dansi. Baada ya serikali kuvunja Vyama vya Ushirika na kuamuru kila mkoa ujitegemee, CUT ikaamua kuja na mtindo wa kuiunda au kuikusanya bendi hiyo kila mwaka inapokaribia sikukuu ya Wakulima (Nane Nane), ambao walikuwa wakiwashawishi baadhi ya wanamuziki waliopata kuimbia bendi hiyo na kwenda kwenye sherehe hizo. Hata hivyo, juhudi hizo zilikoma mwaka mwaka 1996 na mpaka sasa hakuna anayeikumbuka. Imekufa kama zilivyokufa Urafiki Jazz, UDA Jazz, Bima Lee Orchestra, na nyinginezo zilizokuwa zikimilikiwa na mashirika ya umma.