Top 10 similar words or synonyms for kinachofaa

NotFoundError    0.789

Top 30 analogous words or synonyms for kinachofaa

Article Example
Vihisishi Kila kihisishi huweza kuibua hisia mahususi. kwa hiyo ni vyema kutumia kihisishi kinachofaa.
Mali (Kipindi cha Runinga) MALI ni hadithi ya tamaa ya kufanya kinachofaa na mambo yote yanayohusu mwendo huo. MALI inapeleka mtazamaji katika mwendo wa kuonyesha dubwana za jamii hiyo, jamaa na umbali mtu anaweza kuenda katika kutafuta mapenzi, pesa na furaha iliyoje.
Dawa za mfadhaiko Uteuzi wa dawamfadhaiko na kipimo kinachofaa kwa tukio fulani na mtu fulani ni mchakato mrefu na wenye utata, unaohitaji maarifa ya mtaalamu. Baadhi ya dawamfadhaiko yanaweza kutibua mfadhaiko katika siku za awali, yanaweza kusababisha wasiwasi, au wanaweza kumfanya mgonjwa awe na fujo, dhiki au ahisi sana kujiua. Katika matukio chache, dawamfadhaiko inaweza kusababisha kubadilika kutoka mfadhaiko hadi wazimu au haipomania.
Utunzi wa wanyama wa nyumbani Shirika la kuwalinda wanyama huwa zinaangalia sana kwamba mnyama asiteswe lakini aangaliwe vizuri, apewe chakula kinachofaa, alazwe mahali pema palipo joto na pasipo unyevu, atibiwe iwapo ana ugonjwa wowote. Unapopatikana ukitesa mnyama, unaweza ukakuchukulia hatua kali ya kisheria, kutozwa faini, kupokonywa mnyama mwathiriwa au hata kufungwa jela kwa kosa hilo.
Unene wa kupindukia Chakula bora namazoezi ya mwilindiyo njia kuu za kutibu unene wa kupindukia. Ubora wa chakula unaweza kuimarishwa kwa kutumia vyakula vilivyo na nguvu nyingi, kama vile vyakula vilivyo na kiwango cha juu cha mafuta na sukari, na kwa kutumia unyuzi wa chakula kwa wingi zaidi. Dawa za kukabiliana na unene wa kupindukiazinaweza kutumiwa kupunguza hamu ya chakula au kuzuia ufyonzaji wa mafuta, huku mtu akila chakula kinachofaa. Iwapo chakula bora, mazoezi na matibabu hayatoshi, mpira wa utumboni unaweza kusaidia kupunguza uzito wa mwili, auupasuaji unaweza kufanywa ili kupunguza ukubwa wa tumbo na/au urefu wa matumbo. Upasuaji huu hupelekea mtu kushiba upesi na kupunguza uwezo wa kufyonza virutubishi vilivyo katika chakula.
Libido Libido (yaani nyege au ashiki) ni uchu au hamu ya kujamiana ambayo hupatikana kwa wanaume na kwa wanawake. Neno hili la Kilatini hutumika hasa mtu alipo na kiwango kidogo cha libido. Hapo ndipo utakaposikia kwamba fulani ana libido kidogo ama mwanamume fulani amekosa nguvu za kiume. Hata hivyo, yafaa ijulikane kwamba kuna tofauti kati ya hamu ya ngono na nguvu za kiume. Mwanamume asiye na nguvu za kiume huenda akawa na kiasi cha libido kinachofaa, lakini hawezi kujamiana na mwenziwe kwa njia inayofaa maana mwili wake hauitikii.
Tiba asilia ya homoni BHRT kwa mara nyingi inahusishwa na upimaji wa mate kwa lengo la kuweka viwango vya chini vya homoni, na kuchanganywa kwa dutu hizo na wanafamasia, kwa ushauri wa madaktari, kuzalisha maandalizi na viwango vya damu vya homoni ambavyo ni binafsi kwa kila mgonjwa. Hakuna utafiti unaonyesha kuna faida yoyote aidha ya matibabu haya. Ingawa watetezi wa BHRT wanadai kwamba upimaji mate kunaweza kutumika ili kuweka kiwango cha homoni "kinachofaa" kwa watu binafsi, na vipimo vinatumiwa kuamua ni homoni gani zinatakiwa kupunguzwa na zinazohitaji nyongeza, hakuna msingi wa kisayansi wa kuunga mkono matumizi ya kupima mate kwani estrojeni inazalishwa mwilini kwa mipapatiko katika ndani na kati ya siku inayosababisha viwango tofauti vya mate. Baadhi ya michanganyiko ya kuchanganya pia hujaribu kutumia kiwango kimoja kwa wanawake wote, bila ushahidi kwamba kiwango maalum kina faida katika kesi zote na bila utambuzi kwamba wanawake wana unyeti tofauti kwa viwango tofauti vya homoni viwango vya kimetaboliki. Kufaaisha hakuelezei athari na kusanasiwa kwa homoni ambako hutokea ndani ya tishu kuliko ndani ya damu, na hivyo viwango vya homoni katika mate au damu si lazima zionyeshe shughuli halisi kibayolojia. Matatizo mengine ni pamoja na ukosefu wa ushahidi kuonyesha kwamba sampuli ni imara wakati wa uhifadhi na usafirishaji, uwezo mdogo wa kurudia matokeo, na tofauti kubwa kati ya tafiti. Pia hakuna utafiti wa kushirikisha dalili na viwango vya homoni katika damu au mate. FDA inapendekeza badala yake kurekebisha tiba ya homoni kulingana na dalili za mgonjwa, na hakuna sababu ya kufanya marekebisho viwango vya dawa au kufuatilia wagonjwa wanaopokea BHRT. Wakosoaji wa BHRT pia wamesema kuwa pia hakuna uhakika kuhusu kile kiwango cha homoni kinachofaa hupatikana mwilini. Shirika la waliomaliza hedhi la Merikani ya Kaskazini wameunga mkono maonyo kuhusu uwezekano wa madhara yanayoweza kusababishwa na BHRT , kwani inafanya misombo ya dawa ambazo tayari zimeidhinishwa na FDA kwa njia ambazo zinakosa ushahidi wa msingi juu ya usalama au madhara, onyo linaloungwa mkono na jamii ya Madaktari wa Uzazi na Wanajinokolojia wa Kanada.
Umaskini Mifano ya nchi zilizo na uongozi bora unaoleta meandeleo ya kiuchumi na kupunguza umaskini ni kama Thailand, Taiwan, Malaysia, Korea ya Kusini na Vietnam, ambazo kwa kawaida huwa na serikali thabiti. Nchi hizi pia zinajulikana kama "nchi ngumu" au "nchi za maendeleo." Hizi “nchi ngumu” zina nia na uwezo wa kuunda na kuweka sera zitakazoleta maendeleo ya muda mrefu yatakayowasaidia wananchi wote, sio tu matajiri. Kampuni za kimataifa hudhibitiwa ili kuhakikisha ya kuwa zinafuata kanuni zinazofaa kuhusu malipo na ajira ya wafanyakazi, zinatozwa ushuru kwa kiwango kinachofaa ili kuleta maendeleo nchini na sehemu ya faida hubaki katika nchi hizo.Faida hii huwekezwa tena ili kusaidia katika maendeleo ya nchi. Katika mwaka wa 1975, nchi ya Korea Kusini ilikuwa na Pato la chini la Kitaifa kwa kila mtu ikilinganishwa na Ghana, na kufikia mwaka wa 2008, ilikua kwa kiwango cha mara 17 ya kile cha Ghana.